Maandazi ni moja ya kitafunwa maarufu sana Tanzania. Pika maandazi na uweze kufungua kinywa kwa maandazi ya mayai na maziwa. Haya maandazi yanaweza kunywewa chai, juice na pia kahawa.
Mahitaji
1.Unga wa ngano ½ kilo
2.Sukari 200g (kikombe kimoja cha chai)
3.Chumvi ½ kijiko kidogo (cha chai )
4.Hamira kijiko 1 kidogo
Yai 1
5.Maziwa ya unga vijiko 2 vikubwa
6.Butter kijiko 1 kikubwa
7..Hiliki kijiko1 kidogo
8.Maji ya uvuguvugu ya kukandia
9.Mafuta ya kuchomea lita 1
10.Kibao cha kusukumia unga wa ngano
11.Sinia au ubao ulionyooka
Maelekezo
Weka unga kwenye bakuli kisha ongeza sukari, chumvi, yai, maziwa ya unga, butter na hiliki. Changanya viambato mpaka mchanganyiko uwe sawia.
Ongeza maji ya uvuguvugu kiasi kwenye mchanganyiko na uanze kukanda. Ni vizuri kukanda mchanyiko huu kwa muda wa dakika 15 ili kuhakikisha donge lote la unga limelainika vizuri.
Gawanya unga uliokwandwa katika madonge manne (4) tofauti.
Weka unga wa ngano kidogo katika kibao cha kusukumia na uanze kusukuma donge moja katika shape ya chapati.
Katika kusukuma, hakikisha unga wako uko wa wastani – siyo mwembamba sana wala mnene.
Ukimaliza kusukuma kata unga kutokana na umbo upendalo kupika maandazi na uyatandaze katika ubao au sinia lililonyooka. Hakikisha sinia au ubao umenyunyuziwa unga wa ngano ili kuzuia unga utakaoweka usingandie.
Rudia hiyo hatua kwa madonge yote yaliyobakia.
Ukimaliza kuandaa maandazi yako, weka maandazi yako katika sehemu iliyokuwa na joto ili yaweze kuumuka.
Hii inaweza kuchukua hadi masaa 3 ili hamira kuumua vizuri unga wako.
Unga ukishaumuka, bandika sufuria, au kikaangio pamoja na mafuta jikoni. Hakikisha mafuta ni mengi ili kuwezesha maandazi kuiva vizuri.
Mafuta yakishachemka tumbukiza mandazi. Acha maandazi kwenye mafuta mpaka yabadilike rangi na kuwa ya brown.
Maandazi yakishaiva, ipua na weka kwenye chujio ili kukausha mafuta. Rudia hatua hizi kwa maandazi yote yaliyobaki.
Subiri yapoe na yako tayari kuliwa.
Inno Mishamo
No comments: