Mapishi Ya wali na stuffed Pepper
Mapishi ya Wali na stuffed pepper
Mahitaji
Pilipili hoho (Red pepper 3)
Cougette 1
Kitunguu (onion 1)
Uyoga (mashroom 1 kikombe cha chai)
Carrot 1
Nyanya (fresh tomato 1)
Nyanya ya kopo iliyosagwa (tomato paste 3
vijiko vya chai)
Giligilani (fresh coriander)
Binzari manjano (Turmaric 1/2 ya kijiko cha chai)
Curry powder 1/2 ya kijiko cha chai
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Kata hoho kati na utoe moyo wake kisha ziweke pembeni, Kisha katakata cougette, kitunguu, uyoga, carrot, nyanya katika vipande vidogo vidogo,
Weka sufuria jikoni na uanze kupika uyoga kwa muda wa dakika 5, kisha weka curry powder,
turmaric na chumvi na kaanga kidogo kisha weka vegetable zilizobakia pamoja na nyanya ya kusaga pamoja na giligilani. Zikaange kwa muda
wa dakika 5 kisha zitie kwenye hoho na kisha uzibake kwa muda wa dakika 20 na hapo zitakuwa tayari kuseviwa na wali.
No comments: