MAPISHI YA MCHEMSHO WA NDIZI NA NYAMA

Mapishi ya Mchemsho wa ndizi na nyama
Mahitaji

Ndizi mbichi 6
Nyama ya ng'ombe (nusu kilo)
Viazi mviringo 2
Kitunguu swaum
Tangawizi
Kitunguu maji
Nyanya 1 kubwa
Mafuta (vegetable oil)
Chumvi
Limao
Pilipili


Matayarisho

Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa



Chef Inno Mishamo 

MAPISHI YA MCHEMSHO WA NDIZI NA NYAMA MAPISHI YA MCHEMSHO WA NDIZI NA NYAMA Reviewed by Unknown on 12:49 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.