Chef Mishamo
➡Mapishi ya Tambi za sukari
Mahitaji
Tambi (spaghetti 1/2 ya packet)
Mafuta (vegetable oil)
Sukari (sugar 1/2 kikombe cha chai)
Hiliki (cardamon 1/2 kijiko cha chai)
Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai)
Tui la nazi (coconut oil 1 kikombe cha chai)
Maji kiasi
Matayarisho
Tia mafuta kiasi kwenye sufuria kisha ibandike jikoni (katika moto wa wastani) yakisha pata moto kiasi tia tambi na uanze kuzikaanga kwa kuzigeuzageuza kila mara mpaka zitakapokuwa za yangi ya light brown. baada ya hapo ipua na umwage mafuta ya kwenye tambi (bakiza kidogo sana kwani usipofanya hivyo tambi zitakuwa na mafuta sana) Baada ya hapo zirudishe jikoni na kisha utie hiliki, chumvi, sukari, tui la nazi na maji kiasi. Zifunike kisha ziache zichemke mpaka maji yakauke. Baada ya hapo zigeuze na uzipike mpaka ziive. Nahapo zitakuwa tayari kwa kuliwa
Posted by Inno Mishamo
No comments: